Dodoma FM

Serikali kuzitumia ripoti za uwajibikaji kukuza utawala bora

28 June 2023, 4:25 pm

Naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akizindua ripoti za uwajibikaji. Picha na Wajibu.

Taasisi ya Wajibu wamezindua Ripoti za Uwajibikaji ambapo ni nne ikiwemo Ripoti ya viashiria vya Rushwa, ubadhirifu na Udanganyifu katika Taasisi za Umma, Ripoti  ya uwajibikaji wa Vyombo vya Usimamizi kwa Taasisi za Umma.

Na Seleman Kodima.

 Naibu katibu mkuu wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, amewahakikishia watanzania kuwa wataendelea kuzithamini  ripoti za uwajibikaji zinazotolewa na taasisi ya wajibu kupitia idara zao hali ambayo itasaidia kukuza uwazi ,uwajibikaji na utawala bora.

Hayo ameyasema wakati akizundua Ripoti za Uwajibikaj  zinazoangazia ripoti ya CAG kwa mwaka 2021/2022 ambapo amewataka Wajibu kuona umuhimu wa kuandaa siku maalum ya kuwasilisha mapendekezo hayo na uwepo wa majadiliano ya pamoja .

Sauti ya  naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

Aidha amesema serikali imeendelea kufanyia kazi taarifa za CAG kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zote za umma na halmashauri ambapo imejielekeza kuhakikisha wanazifanyia kazi taarifa hizo kwa lengo la kuboresha utendaji na kuleta tija kwa serikali.

Sauti ya Naibu katibu mkuu wizara ya Fedha na Mipango.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akizungumza katika uzinduzi huo. Picha na Wajibu.

Awali mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Wajibu amesema ripoti hizo ambazo wamezindua zimeandaliwa kwa lugha rahisi na viwango zinavyohitajika ili kufikia ubora wenye tija.

Sauti ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Wajibu.

Hapo jana Taasisi ya Wajibu wamezindua Ripoti za Uwajibikaji ambapo ni nne ikiwemo Ripoti ya viashiria vya Rushwa, Ubadhirifu na Udanganyifu katika Taasisi za Umma, Ripoti  ya Uwajibikaji wa Vyombo vya Usimamizi kwa Taasisi za Umma, Ripoti ya Uwajibikaji ya Usimamizi wa Mapato na Matumizi na Ripoti ya Uwajibikaji, Utoaji wa Huduma kwa Jamii.