Dodoma FM

Wasomi washauriwa kutokuchagua kazi

24 May 2023, 6:05 pm

Katika picha ni Bw. Peter Mtandika akihudumia miche katika Bustani yake. Picha na Bernad Magawa.

Peter ametoa wito kwa vijana kupambana bila kuchagua kazi ilimradi iwe halali na isiyo na madhara kiafya.

Na Bernad Magawa .

Vijana wasomi wilayani Bahi mkoani Dodoma wameshauriwa kuacha kuchagua kazi za kufanya badala yake wajikite katika kutengeneza ajira binafsi ili kujikwamua kiuchumi badala ya kusubiri kuajiriwa na serikali.

Hayo yamesemwa na Peter Mtandika, kijana aliyejiajiri katika bustani ya kuotesha miche ya miti kwa lengo la kujipatia kipato lakini pia kuhakikisha anashiriki katika kuboresha mazingira ya wilaya ya Bahi.

Sauti ya Peter Mtandika.
Mwonekano wa miti iliyooteshwa na Bw. Peter . Picha na Bernad Magawa.

Pamoja na mafanikio ya kujipatia kipato, Peter amesema kwa kiasi kikubwa anaona fahari kwa kushiriki katika kazi za kutunza mazingira kwani amekuwa akisambaza miche hiyo maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na baadhi ya idara za serikali.

Sauti ya Peter Mtandika.

Peter ametoa wito kwa vijana kupambana bila kuchagua kazi ilimradi iwe halali na isiyo na madhara kiafya kwani dunia kwa sasa ipo katika wimbi kubwa la vijana wengi kutokuajiriwa na serikali .

Sauti ya Peter Mtandika.