Dodoma FM

Serikali yataka mapendekezo sheria ya sauti zinazozidi katika nyumba za ibada

13 June 2023, 12:39 pm

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa wakati akifungua kongamano la kitaifa la kuwajengewa uelewa viongozi wa dini.Picha na Fred Cheti.

Kongamano hilo lina lengo la kujadili na kuwajengea uelewa viongozi wa madhehebu ya dini nchini juu ya kufahama athari zinazoweza kutokana na kelele na mitetemo katika nyumba za ibada ili wakawe mabalozi kwa waumini wao.

Na Fred Cheti.

Serikali imewataka viongozi wa madhehebu yote ya dini kupitia jumuiya ya Maridhiano ya amani nchini (JMAT) kwa kushirikiana na NEMC kufanya mapitio ya  sheria la suala la  sauti zinazozidi katika nyumba za ibada na kutoa mapendekezo yao.

Maagizo hayo yametolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa wakati akifungua kongamano la kitaifa la kujengewa uelewa kwa viongozi wa dini juu ya athari za sauti zilizozidi katika jumba za ibada lililoandaliwa na Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na jumuiya ya Maridhiano ya Amani nchini (JMAT)

Sauti ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa .
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Jaffo akizungumza katika kongamano hilo. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Jaffo anaelezea azma ya serikali katika jambo hilo.

Sauti ya Dkt Selemani Jaffo .

Nae Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya Maridhiano  ya amani nchini (JMAT)Dkt.Alhad Mussa  amezungumzia malengo ya jumuiya hiyo kwa kushirikaina na serikali katika jambo hilo.

Sauti ya Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya Maridhiano .