Dodoma FM

Watakiwa kujitokeza kupata msaada wa kisheria

5 May 2026, 15:56

Picha ni wasaidizi wa msaada wa kisheria wakitoa msaada kwa wananchi. Picha na Mtandao.

Amesisitiza wananchi kuwa wa kweli,wawazi na wenye uhakika na kile watakacho kwenda nacho kupata msaada wa kisheria .

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Iyumbu na Ihumwa wametakiwa kutumia vyema fursa ya msaada wa kisheria za Mama Samia kampeni ya awamu ya pili ambayo imeanza tangu Mei1 ikitarajiwa kufungwa Mei 15.

Wito huo umetolewa na mhudumu wa jamii (community case worker) Bi.Mariam Maswaula ambapo amewataka wananchi wote wenye changamoto mbalimbali za ndoa, mirathi na ardhi kujitokeza ili kupata msaada wa kisheria.

Aidha amesisitiza wananchi kuwa wa kweli,wawazi na wenye uhakika na kile watakacho kwenda nacho kupata msaada wa kisheria .

Sauti ya Bi.Mariam Maswaula .

Bi.Maswaula ameongeza kuwa huduma hiyo ni bure hivyo hakuna mashaka ya kuhofia kutozwa gharama yoyote kwani lengo la kampeni hiyo ni kupunguza na kuondoa migogoro mbalimbali ndani ya jamii.

Sauti ya Bi.Mariam Maswaula .

Nao baadhi ya wakazi wa Iyumbu wamempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan Kwa juhudi za kuleta amani kwa wananchi kupitia msaada wa kisheria ambao nje na Sheria lakini unatoa elimu ya mambo mbalimbali yahusuyo familia na malezi bora

Sauti za wananchi.