Dodoma FM

Leo tunaangazia umri upi sahihi kwa kijana kuwania nafasi za uongozi wa serikali za mitaa

18 March 2024, 6:43 pm

Mtu anayetaka kugombea nafasi hizo awe na umri wa miaka ishirini na moja au zaidi. Picha na UN.

Hizo ni sifa chache tu, lakini leo tumezungumza na mwanamke ambaye ni kiongozi wa serikali ya mtaa wa Mpamaa ili kujua ilikuwa rahisi au ngumu kiasi gani yeye kuwania nafasi hiyo hadi kuwa kiongozi.

Na Seleman Kodima.
Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, ngazi ya vijiji/mitaa na Vitongoji 2019 inaweka wazi sifa za mgombea wa nafasi hizo ambapo moja ya sifa ni pamoja na mtu anayetaka kugombea nafasi hizo awe na umri wa miaka ishirini na moja au zaidi na pia awe mkazi wa mtaa, kijiji na kitongoji husika.