Dodoma FM

Uhaba wa maji Suguta ni kikwazo cha ndoa nyingi

31 May 2022, 1:30 pm

Na;Mindi Joseph .          

Wananchi Kijiji cha Suguta wilayani kongwa wameiomba serikali kuwatatulia changamoto ya maji ambayo inawakabili kwa Muda mrefu.

Taswira ya habari imezungumza na Baadhi ya wanawake ambapo wamesema wamekuwa wakilazimika kukaa kisima kwa muda mrefu wakisubiria kuchota maji.

Wameongeza kuwa hali hii imechangia ndoa kuvunjika na kuzaa watoto nje ya ndoa.

.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya kongwa Remidius Mwema amewataka wananchi wanaofanya shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji kuacha mara moja.

.

Changamoto ya maji Mkoani hapa Bado inayakabili maeneo mbalimbali hususani vijijini hivyo jitihada za serikali zinahitajika ili kuwatua ndoo kichwani wanawake.