Dodoma FM

Waiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kujengewa daraja

21 February 2023, 12:17 pm

Wakazi wa kata ya Dabalo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwajengea daraja.Picha na Martha Mgaya

Wakazi wa kata ya Dabalo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwajengea daraja linalounganisha baadhi ya vijijini katika kata hiyo.

Na Fred Cheti.

Wakazi wa kata ya Dabalo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwajengea daraja linalounganisha baadhi ya vijijini katika kata hiyo.

Dodoma Tv ilifika katika kata hiyo na kuzungumza na baadhi ya wananchi ambao wamesema changamoto hiyo imekuwa ya muda mrefu kutokana na miundombinu ya daraja hilo kuwa ya zamani.

Aidha wananchi hao wamesema daraja hilo limekuwa likisababisha maafa mara kadhaa ikiwemo watu kupoteza maisha wakati wakijaribu kuvuka pindi linapojaa maji.

Sauti za Wananchi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Dabalo wilayani humo Bwn. Omary Kiguma amekiri kuwepo kwa changamoto ya daraja huku akieleza mipango na hatua zilichokuliwa mpaka sasa kukabiliana na changamoto hiyo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Dabalo Omary Kiguma.