Dodoma FM

Chama cha mafundi kuboresha mazingira ya kazi zao Dodoma

7 November 2023, 3:42 pm

Picha ni mafundi waashi jijini Dodoma wakiendelea na kazi ya ujenzi wa nyumba. Picha na Yussuph Hassan.

Ufundi ni moja kati ya tasnia yenye mchango mkubwa katika kuanzisha ukuaji wa miji.

Na Yussuph Hassan.

Imeelezwa kuwa uwepo wa chama cha mafundi rangi na ujenzi Mkoani Dodoma itasaidia kwa kiasi kuboresha mazingira ya kazi kwa mafundi hao.

Kutokana na shughuli zinazofanywa na mafundi, kundi hilo ni kama limesahaulika, kulingana na mafundi mbalimbali wakizungumza na taswira ya habari wanakiri kundi hilo kuachwa nyuma lakini pia wanakumbana na changamoto lukuki kazini.

Sauti za mafundi.
Picha ni Waziri wa Madini Mh. Antony Mavunde alipata fursa ya kuzungumza na kundi hilo.

Kwa kutambuwa umuhimu kundi hilo kampuni ya ujenzi Magic Builder International, inawakutanisha mafundi rangi na ujenzi kutoka Dodoma kwa ajili ya uanzshiwaji wa chama cha mafundi ambapo Mbunge wa Dodoma na Waziri wa Madini Mh. Antony Mavunde anapata fursa ya kuzungumza na kundi hilo.

Sauti ya Mh. Antony Mavunde.

Kwa upande wake Mlezi wa chama cha mafundi kutoka kampuni ya Magic builder  David Barongo anabainisha lengo la mkutano huo na mafundi rangi na ujenzi Dodoma.

Sauti ya David Barongo .

Sanjari na hayo kampuni ya vifaa vya ujenzi ya Magic Builder International imetoa zawadi kwa washiriki na washindi mbalimbali ikiwemo, vyeti, Pikipiki mbili pamoja na simu za Mkononi.