Dodoma FM

Vijana watakiwa kugeukia kilimo ili kuboresha uchumu

5 April 2023, 3:39 pm

Vijana wakiandaa shamba kwaajili ya kilimo.Picha na Mindi Joseph.

Vijana wanapaswa kugeukia kilimo kwa kuzingatia mikakati ya serikali iliyopo.

Na Mindi Joseph.

Asasi zisizo za kiserikali zimeendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha vijana wanajihusisha na kilimo cha mazao mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi.

Taswira ya habari imezungumza na wadau wa asasi hizo ambapo wamesema wanaendelea kuwaandaa vijana kujihusisha na kilimo ili kuboresha uchumi wao.

Sauti za wadau wa kilimo
Kilimo cha nyanya. Picha na Mindi Joseph.

Waswahili wanasema jembe halimtupi mkulima hivyo vijana hususani wasomi wanapaswa kuondoa hofu kuingia katika kilimo kwani kinalipa tofauti na wengi wanavyofikiri.