Dodoma FM

Berege: Madereva malori wapatiwe elimu ya kujilinda dhidi ya kemikali

25 May 2023, 7:10 pm

Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri Bi. Pendo Berege akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo hayo. Picha na Fred Cheti.

Ameiomba serikali kutumia nguvu kubwa ya kulinda sekta ya uchukuzi Ili iendelee kuajiri madereva.

Na Fred Cheti.

Wito umetolewa kwa wamiliki wa malori nchini kuhakikisha madereva wao wanapewa elimu kwa ufasaha Ili waweze kujilinda na wasipate madhara wakati wa usafirishaji wa kemikali.

Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri Bi.Pendo Berege ametoa wito huo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya madhara ya kemikali kwa viongozi wa vyama vya madereva katika ukumbi wa jengo la mkemia mkuu wa serikali  jijini Dodoma.

Sauti ya Msajili Wa vyama vya Wafanyakazi .

Aidha Bi. Berege amesema matarajio yake baada ya mafunzo hayo madereva wataweza kuzingatia taratibu za kisheria za utoaji wa taarifa zinazohusiana na masuala ya sumu na kemikali na pia watazingatia usafirishaji salama wa kemikali.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwafatilia mafunzo hayo. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha madereva Tanzania (TADWU) Bw. Schubert G. Mbakizao amesema wao kama viongozi wa madereva kazi yao ni kuhakikisha kwamba wanalinda vyanzo ambavyo vinaweza kusapoti serikali iweze kuviendeleza hususani kwenye bandari.

Sauti ya mwenyekiti wa chama cha madereva.