Dodoma FM

ANSAF:Asilimia 10 pekee ya vijana yajihusisha na kilimo nchini kati ya 65

3 December 2020, 2:56 pm

Waziri mkuu mstahafu Mizengo Pinda(wa kwanza kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (wa pili kulia) wakikagua bidhaa za wajasiriamali wa kilimo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kujadili fursa za ajira kwa vijana jijini Dodoma lililoandaliwa na ANSAF

Na,Mariam Matundu,

Dodoma.

Sekta ya kilimo ,viwanda na miundombinu zimetajwa kuwa na ufanisi wa kutosha katika kuondoa umasikini na njaa ukilinganisha na sekta zingine za kiuchumi hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda wakati akihutubia katika mkutano wa mwaka wa kujifunza ulioandaliwa na jukwaa la wadau wa kilimo wasio wa kiserikali (ANSAF ) hii leo jijini Dodoma .
Amesema ili kuwa na uchumi wenye ushindani na endelevu ni muhimu kuwekeza katika sekta hii na kutoa kipaumbele kwa kundi la vijana katika uzalishaji.

Awali Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya amesema katika kuhakisha vijana wanavutiwa kujikita katika sekta ya kilimo wizara inatekereza mikakati mbalimbali ikiwemo mkakati wa Taifa wa vijana ambao umetengeneza mazingira wezeshi ya upatikanaji wa rasilimali.
Kwa upande wake mkurugenzi wa ANSAF Audax Rukonge amesema wadau mbalimbali wa kilimo wanawajibu wa kuhakikisha wanajenga uelewa juu ya fursa za ajira kwa vijana kwenye sekta ya kilimo.

Jukwaa la wadau wa kilimo wasio wa kiserikali ANSAF linafanya mkutano wa mwaka wa kujifunza umeanza kufanyika tangu mwaka 2006 na kwa mwaka huu mkutano huu utajadili fursa za ajira kwa vijana katika kilimo kupitia uchumi wa viwanda.