Dodoma FM

Wito watolewa kwa vijana wa vyuo vikuu

4 February 2023, 5:53 pm

Shirika la Msalaba Mwekundu.Picha na Fursa Kazi

Wito umetolewa kwa jamii hasa vijana wa vyuo kujijengea uwezo wa kusaidia kutoa huduma ya kwanza pindi yanapotokea majanga ili kuokoa maisha ya wahanga waliopata matatizo mbalimbali ikiwemo ajali

Na Fred Cheti.

Wito huo umetolewa na Gofrey Mutasilwa Mratibu wa Mtandao Shirika la Msalaba Mwekundu kwa vijana wa vyuo vikuu Dodoma wakati akifanya mahojiano juu ya ushiriki wa vijana katika kuokoa maisha kupitia mafunzo yanayotolewa na shirika hilo la Msalaba Mwekundu.

Sauti ya Gofrey Mutasilwa.

Miongoni mwa shughuli zinazosimamiwa na shirika hilo la Msalaba Mwekundu ni pamoja na uchangiaji Damu ambapo kwa mwezi huu wa pili limeaanda kampeni ya uchangiaji wa damu katika maeneo mbalimbali kama anavyobainisha Bwn James Kibwana mwanachama wa shirika hilo.