Dodoma FM

Jamii imeshauriwa kutumia vyakula mchanganyiko ili kupunguza magonjwa yasiyo na ulazima

5 July 2021, 11:32 am

Na; Shani Nicolous.

Jamii imeshauriwa kutumia vyakula mchanganyiko vya kujenga mwili ili kupunguza magonjwa yasiyokuwa na ulazima pamoja na madhara mengine ambayo yanatokana na uzito wakupindukia.

Akizungmza na Dodoma FM Dr. Mathew kutoka Poly Clinic Jijini Dodoma amesema kuwa kumekuwa na shida mbalimbali kiafya ambazo zimekuwa chanzo cha migogoro katika familia hasa suala la uzazi na asilimia kubwa ya chanzo hicho ni uzito uliopita kawaida.

Ameongeza kuwa ni tatizo ambalo watu wengi hawafahamu chanzo chake hivyo ni vema jamii ikawa na desturi ya kufuatilia afya zao nakutumia vyakula vinavyoshauriwa na wataalamu wa afya pamoja na kufanya mazoezi ikiwa ni pamoja na kuwahi kituo cha afya pindi waonapo mabadiliko hayo.

Kwa upande wao wananchi Jijini hapa wamesema kuwa jamii iache kusubiri wataalamu wa afya kutoa elimu juu ya afya kila siku bali wajijengee utaratibu wa kula vyakula bora na mazoezi yakutosha ili kuepusha migogoro ya familia juu ya afya ya uzazi.

Vyakula vinavyoongeza mafuta mwilini imekuwa ndiyo sababu ya baadhi ya magonjwa mwilini na hata kusababisha ufanyaji kazi wa mwili kuwa mgumu kwa wanawake na wanaume hasa katika swala la uzazi.