Dodoma FM

Ubovu wa barabara Matumbulu wakwamisha zoezi la kuweka nguzo za umeme

24 May 2021, 11:58 am

Na; Benard Filbert.

Kata ya Matumbulu jijini Dodoma inakabiliwa na ubovu wa barabara katika baadhi ya maeneo yake hali inayochelewesha zoezi la uwekaji nguzo za umeme.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa mtaa wa Mkombozi Bw. Haruni Nyakapara wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu maendeleo ya uwekaji wa nguzo za umeme katika eneo hilo.

Amesema kuna wakati zoezi hilo lilisimama kutokana na ubovu wa barabara kwani gari inayobeba nguzo ilishindwa  kupita kusambaza nguzo hizo kutoka na ubovu wa barabara.

Aidha Bw. Harun amesema kuwa  umeme wa REA utawanufaisha wakazi wachache kwani katika kata ya Matumburu kuna miradi miwili ya umeme ikiwa na lengo la kuhakikisha umeme unamfikia kila mwananchi.

Kata ya Matumbulu ni miongoni mwa maeneo  ambayo yatanufaika na umeme wa REA ambao unawaafikia wananchi kwa kulipia gharama kidogo.