Dodoma FM

Baadhi ya wafanyabiashara waeleza jinsi wanavyonufaika

27 February 2023, 1:17 pm

Mfanyabiashara Eric Vumilia Josephat wa soko la sabasaba la jijini Dodoma akielezea jinsi anavyonufaika.Picha na Martha Mgaya

Baadhi ya wafanyabiashara wa matunda katika soko la sabasaba jijini dodoma wameelezea namna wanavyonufaika na biashara ya kuuza matunda.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wa matunda katika soko la sabasaba jijini dodoma wameelezea namna wanavyonufaika na biashara ya kuuza matunda hususani kwa msimu huu ambapo yapo kwa kiasi kikubwa.
Dodom FM imefanya mahojiano na baadhi ya wafanyabiashara wa matunda katika soko hilo ambapo wamesema kuwa uwepo wa biashara hiyo umesaidia kutatua baadhi ya changamoto kwa kuwapa vijana fursa ingawa zipo baadhi ya changamoto.

Biashara ya matunda soko la sabasaba jijini Dodoma.Picha na Martha Mgaya
Sauti za wafanyabiashara.

pamoja na kuwa biashara hiyo imeendelea kuwa na fursa kwao wanasema kuwa gharama za kusafirisha bidhaa hiyo kutoka katika soko la ndugai hadi sabasaba inawapa ugumu hususani katika suala la kulipia jambo linalopelekea kutokupta faida ipasavyo.

Biashara ya matunda.Picha na Martha Mgaya

katika masoko mbalimbali yapo baadhi ya matunda ambayo yameonekana kushamiri kwa msimu huu ikiwemo embe nanasi peasi na matunda damu.