Dodoma FM

Wananchi Membe watarajia kunufaika na kilimo cha umwagiliaji

28 March 2023, 4:46 pm

Ujenzi wa bwawa hilo ukiwa unaendelea katika kijiji cha Membe Jijini Dodoma .Picha na Mindi Joseph.

Na Mindi Joseph

Ujenzi wa Bwawa la kilimo cha umwangiliaji Membe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma umefikia asilimia 35 huku  ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika mwezi Augosti 2023.

Taswira ya Habari imezungumza na Mhandisi Saleh Ramadhan ambaye ni msimamizi mkuu wa ujenzi wa bwawa hilo ambapo amesema bwawa hilo litakuwa na  uwezo wa kuhifadhi maji ujazo wa lita Bilioni 12.

Amesema Ujenzi huo ulianza mwaka 2022 na unatumia miezi 12 ili kukamilika.

Sauti ya Mhandisi Saleh Ramadhan ambaye ni msimamizi mkuu wa ujenzi wa bwawa hilo

Wananchi wanasema watanufaika kutokana na bwawa hilo.

Bwawa hili litakidhi mahitaji ya kilimo cha umwagiliaji ambapo itajengwa pia skimu yenye ekari elfu nane pamoja  na matumizi ya nyumbani.