Dodoma FM

Madiwani wa Dodoma mjini watakiwa kuyaenzi mafanikio waliyo yakuta

6 August 2021, 11:50 am

Na; Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa madiwani wa kata zote za Wilaya ya Dodoma mjini kuyaenzi mafanikio waliyoyakuta katika jiji na namna yakuendeleza uchumi hasa katika zao la zabibu.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh Jabiri Shekimweli wakati akizungumza na katika baraza la madiwani lilofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma.

Amesema kuwa mikakati yake nikuhakikisha zao la zabibu linafanikiwa kadharika kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujiajiri kupitia uchumi wa viwanda.

Amelipongeza baraza hilo la madiwani kwa kutoa wakurugenzi watatu kwa pamoja ambao ni mazao yao hivyo wasiridhike na hatua hizo bali wafanye kazi kwa ufanisi na kwa juhudi ili kuleta maendeleo katika Jiji kwa manufaa ya wananchi na Nchi nzima.

Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma mjini Mh. Antony Mavunde amesema kuwa ahadi yake nikufanya kazi kwa ufanisi yeye pamoja na madiwani na kumpa ushirikiano mkubwa mkuu wa Wilaya ili kufikia malengo kwani wameona muelekeo wake mzuri wa kuleta maendeleo.