Dodoma FM

Kisima cha maji chaleta Neema kwa wakazi wa Farkwa.

28 June 2022, 9:17 am

Na ;Victor Chigwada.

Kupatikana kwa mita ya kisima Cha maji katika Kijiji cha Farkwa imesaidia kupunguza changamoto ya maji katika eneo hilo.

Akizungumza na taswira ya habari Diwani wa Kata hiyo Bw.Stephano Patrick amekiri hali ya upatikanaji wa maji Kijiji hapo kuongezeka licha ya baadhi ya maeneo kuendelea kuwa na uhitaji mkubwa.

.

Bw.Patrick ameongeza kuwa changamoto hiyo inapelekea idadi kubwa ya Vijiji kuendelea kutumia maji ya makorongoni ambayo siyo safi na salama na kuiomba Serikali kuingilia Kati katika utatuzi wa changamoto hiyo.

.

Pamoja na kuwepo jitihada za makusudi zinazofanywa na Serikali na taasisi binafsi ili kutatua changamoto ya maji kwenye maeneo mbalimbali nchini,lakini bado huduma hiyo imeendelea kuadimika zaidi hali inayosababisha adha kubwa kwa wananchi.