Dodoma FM

Serikali yapiga marufuku matumizi ya vifungashio vya plastiki

11 April 2023, 1:00 pm

Waziri wa Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jaffo. Picha na Fred Cheti.

Na Fred Cheti.

Serikali hivi karibuni ilipiga marufuku matumizi yasiyo sahihi ya mifuko  laini ya plastiki kutumika kama vibebeo vya bidhaa huku jambo hilo likitajwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria  ambapo imeahidi  kuwachukulia hatua wanaofanya hivyo

Baada ya tamko hilo la serikali lililotolewa na Waziri wa Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jaffo Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya wananchi jijini hapa ambao wamekua na maoni tofauti juu ya jambo hilo.

Sauti za wananchi
Vifungashio hivyo vya plastiki baada ya kutumika na kutupwa hupelekea uchafuzi wa mazingira. Picha na Fred Cheti.

Serikali imesema kuwa hali ya matumizi yasiyo sahihi ya vifungashio hivyo imekua ikisababisha uchafuzi wa mazingira.

Sauti ya Waziri wa Muungano na Mazingira