Dodoma FM

Kampeni ya uchunguzi wa macho CVT yaendelea

19 January 2021, 2:29 pm

Na,Alfred Bulahya

Dodoma.

Kampeni ya kupima na kufanya uchunguzi wa macho katika hospitali ya macho ya CVT iliyopo Uzunguni Jijini Dodoma, imeendelea leo kwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa 3 waliobainika kukutwa na tatizo la mtoto wa jicho.Hayo yanajiri ikiwa ni muendelezo wa kampeni hiyo iliyopewa jina la Anza mwaka na CVT kwa lengo la kupima na kufanya uchunguzi wa macho bure.Akizungumza na Taswira ya habari hospitalini hapo Daktari anayehusika na zoezi la upasuji Dkt.Nelson Mtajwaa amesema leo Jan 19 wameanza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 3 waliobainika kukutwa na tatizo hilo kufuatia uchunguzi uliofanyika mapema hapo jana.Aidha amesema kuwa wagonjwa wote watatu wamefanyiwa upasuaji kwa kuondoa mtoto wa jicho huku hali zao zikiendelea vizuri.