Dodoma FM

Wakazi wa Mlowa bwawani waipongeza serikali kwa kufanya ukarabati wa barabara

13 January 2022, 2:44 pm

Na; Benard Filbert.

Wakazi wa kata ya Mlowa Bwawani wameipongeza serikali kwa kufanya ukarabati wa baadhi ya barabara katika kata hiyo.

Hayo yameelezwa na wakazi wa kata hiyo wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu hali ya barabara katika kata hiyo.

Wamesema awali barabara zilikuwa hazipitiki hususani msimu wa mvua lakini hivi sasa zimekarabatiwa na zinapitika kirahisi.

Hata hivyo wamesema licha ya ukarabati huo ni vyema serikali ikaongeza nguvu ili ziweze kupitika kirahisi.

Endrew Richard Msea ni diwani wa kata ya Mlowa Bwawani ameiambia taswira ya habari kuwa bado anaendelea kuomba bajeti halmashauri ya Chamwino ili waweze kukarabati barabara zote.

Miundombinu ya barabara ni kichocheo cha maenedeleo kwa wnanchi katika eneo lolote.