Dodoma FM

Wakazi wa Chenene walia na uhaba wa maji

20 October 2022, 12:20 pm

Na; Benard Filbert.

Kusuasua kwa upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji Cha Chenene wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma imetajwa kuwa kero kwa wakazi wa eneo .

Taswira ya habari imefika katika kijiji cha Chenene nakujionea hali halisi ya upatikanaji wa huduma ya maji ambapo imeshuhudia idadi kubwa ya watu wakiwa kwenye foleni katika kituo kimoja kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa upatikanaji wa maji bado ni wakusua sua jambo ambalo linawalazimu kutumia muda mrefu kutafuta huduma hiyo.

.

Hata hivyo wamesema kuwa changamoto nyingine  ni mgao wa maji  ambapo hutumiwa kunywesha wanyama  huku yakiwa na matumizi ya Binadamu.

.

Taswira ya habari inafanya jitihada za kuzungumza na viongozi wa kijiji cha Chenene ili kujua hatua zipi wamechukua kunusuru hali ya wananchi wao katika upatikanaji wa maji safi na salama.