Dodoma FM

Wakazi wa Loje watoa shukrani ujenzi wa Daraja

6 January 2024, 6:02 pm

Wananci hao wameiomba Serikali kuboresha zaidi miundombinu ya daraja hilo ili liweze kudumu na kuwa imara zaidi.Picha na Michuzi blog.

Wananchi hao wanasema kukosekana kwa daraja pia kulihatarisha hali ya usalama wao hasa kipindi cha mvua.

Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kata ya Loje Wilaya ya Chamwino wametoa Shukrani kwa Serikali kwa Juhudi kubwa ya Ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Igunguli na Loje.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wameeleza adha wanayokutanazo wakati wa kuvuka katika eneo hilo.
Aidha wameiomba Serikali kuboresha zaidi miundombinu ya daraja hilo ili liweze kudumu na kuwa imara zaidi.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ingunguli Bw Hamisi Msangi amesema kuwa pamoja na ujenzi huo lakini daraja hilo linatia mashaka kutokana na namna ujenzi ulivyo fanyika .

Sauti ya Mwenyekiti.

Ameongeza kuwa kukosekana kwa kiwango sahihi cha ujenzi kunaweza kusababisha matatizo mengine ya kiusalama.

Sauti ya Mwenyekiti.

Nae Diwani wa Kata ya Loje Bw.John Njohoka ametoa shukrani zake kwa Serikali kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa daraja hilo na kupunguza adha kwa wananchi.

Sauti ya Diwani wa kata ya Loje.