Dodoma FM

Wakazi Chinugulu watembea umbali mrefu kutafuta maji

20 May 2025, 3:24 pm

Wanawake wa kijiji hiki hulazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tatu mpaka nne kutafuta maji kila siku kwaajili ya matumizi ya nyumbani.Picha na Google.

Aidha  umbali uliopo kutoka Kijiji cha Chinugulu mpaka mto Kizito ambako ndipo maji yanapatikana ni hatari kwa wananchi kwani mto huo unatumiwa pia na wanyama waliopo katika hifadhi ya wanyama ya  Ruaha.

Na Victor Chigwada.

Imeelezwa kuwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu mpaka nne umekuwa changamoto kwa wakazi wa Chinugulu Wilaya ya Chamwino pindi wanapohitaji kupata huduma ya maji ya kunywa na matumizi mengine.

Wakizungumza na Taswira ya Habari wameeleza namna ambavyo changamoto hiyo imehatarisha maisha ya akina mama kwani ndiyo wawajibikaji wakubwa wa kutafuta maji.

Aidha changamoto hiyo imekuwa ikiathiri mahusiano ya ndoa kwani baadhi ya wanaume wanashindwa kuamini kuteka maji inaweza kugharimu muda mwingi wake zao.

Ingawa ndiyo uhalisia wenyewe wa kufuata maji ambayo hata hivyo ni maji ya visima na mito hivyo kuna kuwa na msongamano.

Sauti za wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Chinugulu Ndg. Sanjeli Njelula ameeleza namna ambavyo changamoto hiyo imekuwa sugu pasipo na matumaini ya kusaidiwa licha ya kuhangaika kutafuta misaada ya kuchimbiwa kisima bila mafanikio

Sauti ya mwenyekiti