Dodoma FM
Dodoma FM
8 May 2026, 17:05

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Wanu katika nafasi hiyo akisema anamfahamu vizuri na alijua kuwa ana uwezo wa kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi.
Na Mariam Kasawa.
Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mariam Ditopile Mzuzuri, amesema kuanzishwa kwa makambi maalumu ya wanafunzi wa kutwa yamekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia shule hizo kufanya vizuri kitaaluma kama ilivyo kwa shule za bweni.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bungeni jijini Dodoma leo Mei 8, 2026, Mariam amesema mfumo huo umeonesha mafanikio makubwa katika Wilaya ya Kondoa kwa kuwapa wanafunzi mazingira bora ya kujisomea na kujiandaa kwa mitihani.
Ni katika muktadha huo, mbunge huyo ameitaka Serikali pamoja na wadau wa elimu kusaidia makambi hayo kwa kuyapatia mahitaji muhimu yatakayowezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwa ajili ya kujiandaa na mitihani.
Kwa mujibu wa Mariam, uwekezaji katika makambi hayo unaweza kusaidia kupunguza tofauti ya ufaulu kati ya shule za kutwa na zile za bweni.
Katika hatua nyingine, Mariam amempongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri, Wanu Hafidh Ameir, kwa kile alichosema kuwa ni utendaji mzuri katika kusimamia sekta ya elimu nchini.