Dodoma FM

Aga Khan Foundation yaendelea kuyawezesha makundi maalum

6 July 2026, 17:25

Mradi huo wa miaka mitatu unafadhiliwa na Ubalozi wa Ireland na unatekelezwa katika halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma.Picha na Anwary Shaban.

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za kuongeza ushiriki wa makundi maalumu katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha wanapata fursa sawa za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Na Anwary Shaban.

Shirika la Aga Khan Foundation, kupitia mradi wa Tuinuke Pamoja, limeendelea kuwawezesha wananchi wa makundi maalumu mkoani Dodoma kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali yanayolenga kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Akizungumza  jijini  Dodoma, Afisa Mradi kutoka Shirika la Aga Khan Foundation, Erick Kisiga, amesema mradi huo wa miaka mitatu unafadhiliwa na Ubalozi wa Ireland na unatekelezwa katika halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuhimiza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake pamoja na makundi maalumu, hususan watu wenye ulemavu.

Aidha, amesema mafunzo yaliyotolewa leo yamelenga kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu ili waweze kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi zitakazobadili maisha yao pamoja na kubadili mtazamo wa jamii kuhusu uwezo wao.

Mradi huo wa miaka mitatu unafadhiliwa na Ubalozi wa Ireland na unatekelezwa katika halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma.Picha na Anwary Shaban.

Kwa upande wake, Afisa Mradi kutoka Shirika la SEDIT, Mohamed Mahmood, amesema mafunzo hayo ya ujasiriamali yanayoratibiwa na Aga Khan Foundation kupitia mradi wa Tuinuke Pamoja yameandaliwa mahsusi kuwawezesha wajasiriamali kutoka makundi maalumu kwa kuwapa maarifa ya kuanzisha, kusimamia na kukuza biashara zao kwa ufanisi.

Nao wanufaika wa  mafunzo hayo wamesema elimu waliyoipata kutoka Shirika la SEDIT kwa kushirikiana na Aga Khan Foundation itawasaidia kuboresha shughuli zao za kiuchumi, kuendesha biashara kwa tija na kuongeza kipato chao, huku akiishukuru Serikali na wadau kwa kuendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu.

Sauti ya Daniel Njau kina.