Bodaboda wacharazwa vikoko baada ya kukiuka sheria
27 November 2026, 13:03

Katika hatua nyingine, Dodoma fm radio inaendelea na jitihada za kupata ufafanuzi kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, ambaye awali alielezwa kuwa alikuwa kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa, ili kupata kauli ya Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo.
Na Kitana Hamis.
Wananchi wa Kijiji cha Njoro wilayani Kiteto wamelazimika kuchukua sheria mkononi na kuwapa adhabu ya viboko baadhi ya madereva bodaboda waliokuwa wakisherehekea harusi kwa kuendesha pikipiki kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.
Wakiongea na Taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo vinavyohatarisha maisha ya watu huku wakieleza sababu za kutoridhishwa na mwenendo wa madereva hao.
Mmoja wa viongozi wa maafisa usafirishaji almaarufu kama bodaboda ameonesha masikitiko yake kuhusu tukio hilo, akieleza mtazamo wake juu ya hatua iliyochukuliwa na wananchi.

Nao viongozi wa dini ya Kiislamu walio hudhuria harusi hiyo wameelezwa kusikitisha na vitendo vya bodaboda huku umuhimu wa kudumisha amani na kuheshimu sheria.