Dodoma FM

Vijana watakiwa kujali na kuwa thamini wazazi na wazee

5 November 2026, 16:57

Picha ya kijna na mtoto wakionesha heshima na utii wa wakubwa waliwazidi umri. Picha na Dodoma fm

Vijana na watoto wametakiwa kutambua, kuthamini na kuheshimu mchango wa wazazi pamoja na wazee katika jamii kwa kuwajali na kuwapatia msaada wanapouhitaji, hususan wanapofikia umri wa uzee.

Na Victor Chigwada.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mbelezungu wamesema wazazi wengi wamekuwa wakikosa msaada kutoka kwa watoto wao wanapokuwa wazee, hali inayowalazimu kukabiliana na changamoto za maisha bila msaada wa karibu kutoka kwa familia zao.

Wamesema hali hiyo inaonesha umuhimu wa kuwajenga watoto na vijana katika misingi ya upendo, heshima na uwajibikaji kwa wazazi, ili kutambua mchango na malezi waliyoyapata tangu wakiwa wadogo.

Hivyo, wamewataka vijana na watoto kubadili mtazamo kwa kuwapa wazazi na wazee nafasi inayostahili katika maisha yao, kwa kuwajali, kuwaheshimu na kuwasaidia wanapohitaji, kama sehemu ya kudumisha mshikamano na utu katika jamii.

Simulizi na Victor Chigwada.