Dodoma FM

UCSAF kuwafikiwa wananchi katika maeneo yao

18 November 2026, 17:07

Picha ni jengo la ofisi za UCSAF makao makuu jijini Dodoma. Picha na UCSAF.

Wananchi wametakiwa kutumia utaratibu uliowekwa kuwasilisha taarifa, maombi na malalamiko yanayohusu changamoto za mawasiliano katika maeneo yao ili ziweze kufanyiwa kazi na kupata ufumbuzi.

Na Yusuph Hassan.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kanda ya Kati wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Shirikisho Mpunji, kupitia kipindi cha Dodoma Live, ambapo amesema kuna utaratibu maalumu ambao wananchi wanapaswa kuufuata wanapowasilisha changamoto zinazohusu huduma za mawasiliano.

Sauti ya Mkuu wa Kanda ya Kati wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Shirikisho Mpunji.

Aidha, Mpunji amesema UCSAF imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zinazolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za intaneti katika maeneo ya umma, ikiwemo shule, vituo vya afya, vyuo na taasisi nyingine za serikali, hatua inayolenga kuongeza fursa za upatikanaji wa taarifa na kurahisisha matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma.