Dodoma FM

Zaidi ya mita 100 za maji zaibwa Dodoma ndani ya miezi mitatu

27 October 2026, 17:10

Picha ni mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA Mhandisi Aron Joseph akizungumza na waandishi wa habari.

Wizi wa mita za maji ni changamoto inayoweza kuathiri utoaji wa huduma na kuongeza gharama za uendeshaji wa mamlaka za maji, huku ushirikiano kati ya wananchi na watumishi wa huduma hizo ukiwa muhimu katika kuzuia vitendo hivyo.

Na Anwary Shabani.

Ushirikiano hafifu baina ya wananchi na watumishi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA jijini Dodoma umetajwa kuwa chanzo kinacho wizi wa mita kutokana na mita nyingi kufungwa nje ya uzio wa nyumba.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wanannchi ambapo wamesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwapa wakati mgumu wasoma mita wanao pita katika kaya zao jambo ambalo si zuri pia wameiomba serikali kutoa adhabu kali kwa yeyote ataka kamatwa kwa kosa la wizi wa mita za maji.

Octoba 26 2026 akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA Mhandisi Aron Joseph alimesema zaidi ya mita 100 za maji zimeibiwa jijini Dodoma ndani ya miezi mitatu, akitaja wizi huo kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili mamlaka hiyo.

Simulizi na Anwary Shabani.