Wananchi wameipongeza serikali kutoa fedha za ujenzi wa madarasa Dabalo
13 October 2026, 17:01

Wananchi wametakiwa kufahami umuhimu wa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia, ikiwemo miundombinu kam madarasa na vifaa mbalimbali vya kujifunzia ili kumjengea mwanafunzi mazingira salama na rahisi ya kujisomea.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kata ya Dabalo, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, wamepongeza Serikali kwa kutoa fedha zilizowezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Dabalo, hatua iliyosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi.
Baadhi ya wananchi Wamesema awali shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya wanafunzi kuwa wengi katika vyumba vya madarasa, hali iliyokuwa ikileta ugumu katika mazingira ya kujifunzia.
Hata hivyo, wameiomba Serikali kuendelea kusaidia ujenzi wa shule nyingine ya sekondari ulioanzishwa kwa nguvu za wananchi katika Kijiji cha Chiwondo ili kuongeza fursa za elimu katika eneo hilo.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Dabalo, Omary Kiguna, ameipongeza Serikali kwa kutoa zaidi ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, akisema fedha hizo zimechangia kupunguza changamoto ya wingi wa wanafunzi shuleni hapo.