Jela Maisha kwa kumbaka mwanafunzi
17 September 2026, 10:09

Baada ya kusikiliza ushahidi uliowasilishwa mahakamani, Ezra Maziku alikutwa na hatia na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela.
Na Stephen Noel.
Kijana mwenye umri wa miaka 27, Ezra Maziku maarufu ‘Funika’, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka kwa kushirikiana na wenzake mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Pwaga, Wilaya ya Mpwapwa.
Mwendesha mashitaka wa serikali bwana Ahmed Hatibu aliiambia mahakama kuwa mtuhuhumiwa pamoja na wenzanke walitenda kosa Hilo mnamo july 15 2026 Katika kata ya Pwaga wilayani Mpwapwa.
Hukumu hiyo imetolewa Septemba 15, 2026, katika Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Hakimu Yunis Kambole, katika kesi namba 17257 ya mwaka 2026.
Kwa mujibu wa maelezo ya mahakamani, Maziku alidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu 130 (1) (2)A na 131A ya kanuni ya adhabu iliyofaniwa marejeo mwaka 2023, Nikolaus Magomba na Edward Maziku, ambao walitajwa kuhusishwa ya na tukio hilo.
Mwanafunzi huyo, ambaye jina lake limehifadhiwa, alikuwa akisoma Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Pwaga wakati tukio hilo lilipotokea.
Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, familia zilijaribu kutafuta suluhu nje ya vyombo vya sheria, lakini kutokana na mwamko wa jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia, wananchi walipaza sauti na suala hilo kufikishwa katika vyombo vya sheria.