Dodoma FM

Mradi wa maji wa milioni 442 waleta matumaini Nyahanga

21 August 2026, 18:02

Mradi wa maji nyahanga warajiwa kuwa mradi utakao watuawananchi ndoo kichwani. Picha na mtandao.

Mradi huo unatarajiwa kuwekewa jiwe la msingi na mbio za Mwenge wa Uhuru Siku ya tarehe 21 Agosti 2026, ikiwa ni sehemu ya miradi inayotekelezwa kwa lengo la kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

Na Fred Cheti.                                                         

Wananchi wa Kata ya Nyahanga katika Manispaa ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, wameeleza matarajio yao makubwa ya kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kufuatia utekelezaji wa Mradi wa Maji Lugela-Mlimani wenye thamani ya Shilingi milioni 442,243,940.

Wananchi hao wamesema mradi huo ni hatua muhimu katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao, huku wakieleza kuwa wanatarajia kukamilika kwake kutapunguza muda na gharama wanazotumia kutafuta maji.

Akizungumzia mradi huo, Diwani wa Kata ya Nyahanga Josephina Kilimba amesema utekelezaji wake utakuwa na mchango mkubwa katika kupunguza changamoto ya maji katika kata hiyo.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kushirikiana na mamlaka husika katika kulinda miundombinu ya maji ili kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu.

Kwa upande wake, Afisa Mahusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Dkt.John Mukama, amesema mradi wa Maji Lugela-Mlimani unatekelezwa kwa thamani ya Shilingi 442,243,940 ( Milioni 442.2).

Sauti na Stephen.