Dodoma FM

NIDA kuanza usajili wa watoto kuanzia wanapozaliwa

8 September 2026, 17:02

Utaratibu huo utawezesha mamlaka kupata na kuhifadhi taarifa muhimu za wananchi tangu wakiwa watoto. Picha na Peter Paul
Katemi.

Akizungumza na Taswira ya Habari, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema utaratibu huo utawezesha mamlaka kupata na kuhifadhi taarifa muhimu za wananchi tangu wakiwa watoto, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali, hususan huduma za afya.

Na Peter Paul Katemi.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kuanza utaratibu wa usajili wa watoto kuanzia umri wa sifuri, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo bima ya afya na huduma nyingine muhimu, bila kusubiri mtoto kufikisha umri wa miaka 18.

Baadhi ya wananchi wamepongeza hatua hiyo wakisema itasaidia kupunguza muda na usumbufu katika upatikanaji wa huduma, huku wakitaka NIDA kuhakikisha taarifa za watoto zinalindwa na utaratibu huo hautumiki kuwaongezea wananchi gharama zisizo za lazima.

Wananchi wameiomba NIDA kuhakikisha utaratibu huo unatekelezwa kwa ufanisi na unakuwa mwepesi kwa wazazi na walezi, ili kutimiza lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma na uhifadhi wa taarifa za watoto.

Sauti na Peter Paul Katemi.