Dodoma FM

Vijana wenye ulemavu kuhakikishiwa mazingira jumuishi na ajira zenye staha

31 August 2026, 17:51

Serikali imesisitiza kuwa hatua hizo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha vijana wenye ulemavu wanapata fursa sawa za kujenga vipaji, kupata ujuzi, kuajiriwa au kujiajiri.Picha na Bunge.

Dkt. Seif amesema hayo, Agosti 31, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Yumna Omari, aliyetaka kujua mkakati mahususi wa Serikali katika kukuza ujuzi na vipaji vya vijana wenye ulemavu ili kuongeza ushiriki wao katika ajira na elimu.

Na Mariam Kasawa.

Serikali inaendelea kutekeleza mkakati endelevu wa kuhakikisha vijana wenye ulemavu wanapata fursa za ajira zenye staha na mazingira jumuishi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Afya, Dkt. Jafar Seif, ambapo amesema mesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Toleo la mwaka 2024, pamoja na kuunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Dkt. Seif amesema Serikali itaendelea kuboresha mifumo jumuishi katika sekta za elimu, ajira na ufundi stadi, sambamba na kukuza ubunifu na vipaji vya vijana wenye ulemavu.

Aidha, amesema vijana 643 wenye ulemavu wamejiunga na kuhitimu katika vyuo mbalimbali vya ufundi stadi nchini, ikiwemo VETA, hatua inayolenga kuwaongezea ujuzi na kuwaandaa kushiriki kikamilifu katika soko la ajira.

Sauti ya Dkt. Jafar Seif.