Dodoma FM

Vibao vya mitaa vyageuzwa biashara ya vyuma chakavu Mlowa

17 September 2026, 11:27

Picha ni moja ya kibao cha mtaa ambacho kinaeleza majina ya mitaa husika.Picha na Michuzi Blog.

Amesema wanaendelea kufuatilia suala hilo ili waweze kukomesha wizi huo ulio kithiri katika kata hiyo.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa kata ya Mlowa barabarani wamelalamikia tabia ya baadhi ya wananchi kung’oa alama za vibao vya mtaa na kuuza kwenye vyuma chakavu .

Wakiongea na taswira ya habari baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwani wananchi wamegeuza vibao hivyo kuwa biashara huving’oa na kuuza kwenye chuma chakavu hali inayopelekea mitaa kukosa alama.

Wamesema ni vyema Serikali ikadili na wanunuzi wa vyuma chakavu ili kudhibiti upotevu wa vyuma hivyo vya alama za mitaa katika eneo hilo unao tokea mara kwa mara.

Anjero Lukasi Diwani wa Kata ya Mlowa barabarani amekiri uwepo wa  uharibifu wa alama za barabarani ambazo zinakatwa na baadhi ya wananchi wasio kuwa waaminifu nyakati za usiku na kuuzwa kama chuma chakavu.

Ripoti ya Victor Chigwada.