Dodoma FM

Wanawake jitokezeni kupata hati miliki ardhi

3 March 2026, 16:23

Zoezi hili la kliniki ya ardhi limeanza tarehe 2 mwezi March na litahitimishwa tarehe 8 mwezi March. Picha na Jiji la Dodoma.

Serikali ya awamu ya sita imetoa kipaumbele kwa wanawake kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea kupata hati za umiliki wa ardhi.

Na Yusuph Hassan.
Wanawake Mkoani Dodoma wanaomiliki ardhi wametakiwa kujitokeza katika zoezi la kuchukua hati za umiliki kupitia kliniki ya ardhi.

Wito huo umetolewa na Zuhura Mbega mtaalam wa ramani kutoka ofisi ya Kamishna wa ardhi msaidizi Mkoa wa Dodoma. Akizungumza na taswira ya Habari, amesema kuwa kuelekea siku ya wanawake duniani Machi 8 serikali ya awamu ya sita imetoa kipaumbele kwa wanawake kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea kupata hati za umiliki wa ardhi kupitia ofisi zote za ardhi za halmashauri.

Aidha Bi Zuhura amesema kuwa kutokana na mazoea, jamii inaamini kuwa mwanamke hatakiwi kumiliki ardhi, jambo amabalo amesema ni dhana potofu na sio kweli kwani mwanamke naye ana haki stahiki ya kumiliki ardhi na kupata hati yake.

Zoezi hili la kliniki ya ardhi limeanza tarehe 2 mwezi Machi na litahitimishwa tarehe 8 mwezi March kupitia ofisi zote za ardhi katika halmashauri zote Mkoa wa Dodoma.

Sauti ya Zuhura Mbega.