Dodoma FM

Ifahamu maana ya alama ya Ndonye kwa kabila la Wagogo

13 April 2023, 6:33 pm

Mwanamke kutoka katika kabila la wagogo kijiji Msanga akielezea maana ya ndonya. Picha na Fahari ya Dodoma.

Ndonye ilitumika kwa watoto wadogo hapo zamani wa kabila hili la wagogo kama kinga ya macho lakini kwasasa wanasema hawaweki tena alama hiyo.

Na Yussuph Hassan.

Makabila mbalimbali Afrika na Tanzania huwa na alama mbalimbali ambazo hutambulisha kabila hilo kwa watu kuchanja  au kuweka alama hizo katika miili yao.

Kabila la wagodo lilikuwa na alama mbalimbali kama kutoga masikio , kutoa jino pamoja na ndonye wakiamini ni alama na urembo huku ndonye ikiaminika kama kinga ya macho.

Alama hii ya Ndonye huchanjwa katika paji la uso. Picha na Fahari ya Dodoma.