Dodoma FM

Jamii yaomba elimu utambuzi bidhaa zilizothibitishwa na TBS

6 June 2023, 6:11 pm

Wananchi wengi wanadai hawana uelewa juu ya bidhaa zilizothibitishwa na ambazo hazikuthibitishwa na TBS. Picha na Thadei Tesha.

Wametoa wito kwa serikali kupitia shirika hilo kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wananchi pamoja na wafanyabiashara jijini Dodoma wameiomba serikali pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutambua bidhaa kama imethibitishwa na TBS.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma ikiwemo wauzaji pamoja na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali iwapo wanafahamu umuhimu wa kuzingatia alama ya TBS katika bidhaa mbalimbali.

Sauti za wananchi.
Mkazi wa Dodoma akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Kwa upande wake afisa mkaguzi kutoka kitengo cha uthibitishaji bidhaa kutoka TBS makao makuu Bw. Baraka Mbajije anasema kuwa TBS imekuwa ikitoa elimu pamoja na kuwahamasisha juu ya suala la kuzingatia ubora wa bidhaa kwa kuangalia ikiwa imethibitisha na TBS kama navyoeleza.

Sauti ya Afisa mkaguzi kutoka kitengo cha uthibitishaji bidhaa.