Dodoma FM

Madereva watakiwa kujaza mafuta gari ikiwa haina abiria

7 September 2023, 1:56 pm

Picha ni moja ya mabasi yanayo fanya safari mikoa mingine likijazwa mafuta kabla ya kupakia abiria na kuanza safari zake.Picha na Thadei Tesha.

Je sheria hii imatambulika na imekuwa ikifuatwa na madereva wa vyombo vya moto hususani Magari ya abiria.

Na Thadei Tesha.

Madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kutambua kuwa ni  kosa kisheria kujaza Gari mafuta na abiria wakiwa ndani ya gari.

Kauli hiyo imetolewa na CPL.Ester Makali katika mahojiano maalum na Dodoma TV ambapo amesema kuwa ni vyema madereva wakajaza mafuta katika magari yao kabla ya kuanza safari.

Sauti ya CPL .Ester Makali.
Picha ni moja kati ya madereva akiongea na Dodoma Tv kuhusu sheria hiyo ya kujaza mafuta. Picha na Thadei Tesha.

Aidha Dodoma TV imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dodoma ikiwemo madereva juu ya sababu inayochangia baadhi yao kujaza mafuta wakiwa na abiria.

Sauti za baadhi ya wananchi.