

8 August 2023, 5:06 pm
Shirika la Wanawake na Uchumi wa Viwanda Wauvi limekuwa mnyororo wa kuwakutanisha wajasiriamali mbalimbali na kuwapa elimu juu ya ujasiriamali na namna ya kukabiliana na masoko ya kiuchumi.
Na Yussuph Hassan.
Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali Dodoma wanajivunia mafanikio mbalimbali kupitia elimu ya biashara waliyoipata kupitia shirika la wanawake na uchumi wa viwanda Dodoma.
Wameyabainisha hayo wakati wakizungumza na Taswira ya Habari katika maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya nzuguni jijini Dodoma.
Licha ya mafanikio hayo wajasiriamali wameelezea changamoto mbalimbali wanazokabiliana katika shughuli wanazozifanya.
Nao viongozi wa Shirika la Wanawake na Uchumi wa Viwanda WAUVI walikuwa na haya ya kusema.