Dodoma FM

Hali ya upatikanaji wa maji Dodoma kubadilika ifikapo Septemba

7 August 2023, 12:34 pm

Mradi wa Maji Nzuguni unaoendelea kukamilishwa na kampuni ya Helpdesk Engineering Tanzania Ltd. Picha na Seleman Kodima.

Mradi wa maji Nzuguni unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka wastani wa lita mlioni 68.7 mpaka milioni 76.3 kwa siku sawa na ongezeko la 11.4% ya uzalishaji wa sasa, na litapunguza mahitaji kwa 11.7% ya mahitaji ya sasa ya lita 133.4 milioni kwa siku.

Na Seleman Kodima.

Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Mkoani Dodoma DUWASA imewahakikishia wakazi wa Jiji la Dodoma kuwa ifikapo mwezi wa tisa mwaka huu hali ya upatikanaji maji itabadilika tofauti na ilivyo sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Job Masima wakati bodi hiyo ilipotembelea mradi wa Maji Nzuguni unaoendelea kukamilishwa na kampuni ya Helpdesk Engineering Tanzania Ltd ambapo Mradi huo unatarajia kuongeza hali ya upatikanaji wa Maji katika eneo la Nzuguni na maeneo ya Jirani.

Picha ni Mwenyekiti wa Bodi wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Mkoani Dodoma DUWASA ilipotembelea mradi wa Maji Nzuguni unaoendelea kukamilishwa na. Picha na Seleman Kodima.

Balozi Masima amesema kuwa mkataba wa mradi huo unaeleza kuwa mwezi wa nane mwaka huu unatakiwa kukamilika hivyo kipimo sahihi cha ufanisi wao kitaanza Mwezi wa Tisa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Job Masima.

Kwa upande wake Mkurugenzi DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema lengo lao ni kuwahudumia wananchi wa Nzuguni ambapo kipaumbele ni kuhakikisha maji yanatoka .

Sauti ya Mkurugenzi DUWASA Mhandisi Aron Joseph.
Mkurugenzi DUWASA Mhandisi Aron Joseph akizungumza walipo tembelea mradi huo. Picha na Seleman Kodima.

Nae Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa DUWASA Prof, Davis Mwamfupe amewataka wananchi kutumia vyema maji yalipo licha ya Mikakati ya kuongeza upatikanaji wa maji jijini Dodoma kuendelea.

Sauti ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma.