Dodoma FM

Wabunge watakiwa kusimamia pesa za ujenzi wa barabara kuleta maendeleo kwa wananchi

3 August 2021, 1:37 pm

Na;Mindi Joseph .

Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa CCM na Mbunge wa jimbo la Mvumi mkoani Dodoma Mhe Livingstone Lusinde amewaomba wabunge kusimamia fedha walizopewa za kujenga barabara katika majimbo yao kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mh Lusinde amesema kuwa katika bajeti iliyopita kila mbunge wa jimbo la jamhuri ya muungano wa Tanzania wamepatiwa kiasi cha fedha zaidi ya Bilion moja kwaajili ya barabara katika majimbo yote nchini fedha hizo zimeelekezwa kwa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA).

Clip1……..Lusinde

Aidha,Mh Lusinde amebainisha kuwa wao kama wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanakatwa kodi ambazo zinaenda kwenye shughuli za maendeleo hapa nchini.

Clip2..Lusinde

Katika hatua nyingine Mh Lusinde amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa nchini kwa manufaa ya watanzania.