Dodoma FM

Kitabu cha mzee Mwinyi kitakuwa msaada kwa viongozi mbalimbali katika kuhudumia watanzania

10 May 2021, 11:58 am

Na; Benard Filbert.   

Imeelezwa kuwa kitabu kilichozinduliwa hivi karibuni cha Raisi wa awamu ya pili ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi ambacho kinaeleza historia ya maisha yake katika kipindi cha utawala wake kitawasaidia viongozi wa serikali katika kuhudumia watanzania.

Hayo yameelezwa na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma Paul Luisulie wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu kitabu hicho ambapo amesema kitabu hicho kitawasaidia viongozi wengi kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiutawala na kujua jinsi ya kutatua changamoto za wananchi.

Akizungumzia kuhusu gharama kubwa iliyowekwa kwa ajili ya uuzaji wa kitabu hicho amesema ni kutokana na umuhimu wa kitabu hicho kwani ni tofauti na vitabu vingine.

Baadhi ya wananchi wakizungumza na taswira ya habari wamesema ni kweli kitabu hicho kitakuwa na msaada kwa viongozi wa serikali ikiwepo kujua namna bora ya utawala.

Mei nane kilizinduliwa kitabu cha rais wa awamu ya pili wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ally Hassan Mwinyi kinanchoitwa SAFARI YA MAISHA YANGU huku akisherekea kutimiza miaka 96 na mgeni rasmi akiwa rais Samia Suluhu Hassan akiambatana na viongozi wengine.