Dodoma FM

Viongozi ushirika watakiwa kutekeleza kwa vitendo vipaumbele saba

12 September 2023, 1:09 pm

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson, akizungumza na na warajis wasaidizi na watendaji wa vyama vya ushirika jijini Dododma .Picha na Tume ya ushirika .

Kikao kazi kati ya Mrajis na Vyama vya Ushirika vya Upili na Benki ya Ushirika kimefanyika Dodoma kwa siku mbili Septemba 11 na 12 mwaka huu wa 2023 ambapo wadau wamepata fursa ya kutathmini na kujadiliana namna bora ya kuimarisha ushirika nchini.

Na Mariam Matundu.

Viongozi wa vyama vya ushirika nchini wametakiwa kutekeleza kwa vitendo vipaumbele saba muhimu  katika uendeshaji wa vyama vya ushirika  ili kuleta tija katika sekta ya ushirika nchini.

Maagizo hayo yametolewa na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson, septemba 11 mwaka huu wakati akizungumza na na warajis wasaidizi na watendaji wa vyama vya ushirika jijini Dododma .

Akiyataja maeneo hayo saba kuwa  ni: Uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya kidigitali; uanzishaji wa Benki ya Taifa ya  Ushirika; kuhamasisha Mfumo wa Ushirika kujiendesha kibiashara; Usimamizi wa Vyama vya Ushirika; kuhamasisha Ushirika kwenye Sekta mbalimbali na makundi maalum; kushirikiana na wadau mbalimbali kutatua changamoto za Ushirika; na kuimarisha uwekezaji wa Mali za Ushirika katika uzalishaji.

Sauti ya Dkt. Benson.

Amesema iwapo maeneo hayo yatatekelezwa ipasavyo basi itaongeza kasi katika kukuza ushirika na kufanya vyama hivyo kupata hati safi katika kaguzi mbalimbali .

Mmoja wa washiriki katika kikao hichi Biadia Matipa Meneja mkuu wa chama cha ushirika MAMCU amesema wapepokea maagizo ya mrajis na kwamba matumizi ya mifumo ya kidijitali itasaidia kuimarisha ushirika .

Sauti ya Biadia Matipa Meneja mkuu wa chama cha ushirika MAMCU