Dodoma FM

Jamii imetakiwa kuripoti makosa ya jinai yanapotokea na si kujichukulia sheria mkononi

20 October 2021, 11:14 am

Na; Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa jamii kushirikiana na wasaidizi wa kisheria na serikali kuripoti makosa ya jinai yanapotokea kuliko kujichukulia sheria mkononi.

Akizungumza na Dodoma fm kupitia kipindi cha Dodoma live msaidizi wa kisheria kutoka wilaya ya Bahi Daudi Alfred Spilu amesema kuwa mtu akifanya kosa lolote la jinai ni vyema jamii kutafuta wasaidizi wa kisheria na kuripoti katika ofisi za serikali.

Amesema kuwa makosa haya yamekuwa yakileta usumbufu mkubwa kwa baadhi ya watu kwa kukosa haki na hata kupelekea vifo hivyo ni wajibu wa jamii nzima kutokomeza makosa haya na si kupunguza pekee.

Amesema kuwa watu wajue kutofautisha kesi za jinai na kesi za madai kwani kwakutokujua hili usumbufu mkubwa utajitokeza katika kulitatua .

Ameongeza kuwa makosa ya jinai moja kati ya kosa ni kuvunja sheria ya eneo fulani kwa kukusudia.

Mara kadhaa serikali kwa kushirikiana na wasaidizi wa kisheria wamekuwa wkitoa elimu mbalimbali juu ya sheria zinazoihusa jamii kiujumla hivyo jami inapaswa kuzingatia elimu hizo na kuzingatia kwa manufaa yao .