Dodoma FM

Jamii yashauriwa kuzingatia Zaidi matumizi ya Asali

28 August 2023, 12:57 pm

Licha ya asali kuwa na faida nyingi mwilini lakini pia ina madhara endapo matumizi yake yatazidishwa. Picha na Fano product.

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee, kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa Asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na Mdalasini.

Na Abraham Mtagwa.

Licha ya Upatikanaji wa Asali kuwa Mgumu kwa baadhi ya Wananchi lakini jamii imeshauriwa kutumia Zaidi.

Hayo yamefahamika baada ya Taswira ya Habari kuzungumza na baadhi ya watumiaji wa bidhaa hiyo kutoka Jijini  Dodoma ambapo wamesema kuwa, Asali imekuwa na matumizi mengi ikiwemo kutumia kama chakula  na tiba.

Sauti ya baadhi ya watumiaji wa asali.

Bw. Aboutwalib Nassoro ni Mfanyabiashara wa Asali kutoka Soko la Machinga Complex  Jijini Dodoma ametoa ushauri kwa Wananchi kuwa watumiaji wazuri wa Asili licha ya changamoto ya upatikanaji wake.

Sauti ya Bw. Aboutwalib Nassoro.
Picha ni Asali ambayo ipo tayari kwa matumizi . Picha na Mwananchi.

Aidha Taswira ya Habari imefanya mazungumzo na Bw. Beni Majangi ambaye ni Mtaalamu wa Afya kutoka kituo cha Rebohothi Jijini Dodoma, na hapa anaeleza kuhusu  matumizi na faida zinazo patikana katika Asali hasa inapotumiwa kwa usahihi.

Sauti ya Bw. Beni Majangi.

Hata hivyo, Bw. Majangi amebainisha baadhi ya hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi yaliyozidi ya asali katika mwili.

Sauti ya Bw. Beni Majangi.