Dodoma FM
Dodoma FM
27 April 2026, 11:53

Mabadiliko ya tabianchi yanachochea aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na tayari kuna mwenendo ulio dhahiri ambao pasi na shaka unazidi kupanuka kadri janga la tabianchi nchi linavyozidi kuwa baya.
Na Mariam Kasawa.
Ukatili dhidi ya wanawake na wasichan unasalia kuwa kitendo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote, ukiathiri zaidi ya wanawake milioni 1.3, takwimu ambayo hata hivyo haijabadilika kwa zaidi ya muongo mmoja.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women kupitia wavuti wake linasema dharura duniani, majanga, mizozo, na vita vinazidi kuongeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichan na kuchochea visababishi na hatari zaidi.
Mabadiliko ya tabianchi yanachochea aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na tayari kuna mwenendo ulio dhahiri ambao pasi na shaka unazidi kupanuka kadri janga la tabianchi nchi linavyozidi kuwa baya. Kasi ya meandeleo ya teknolojia nayo yanaongeza ukatili wa wanawake na wasichana kupitia mtandaoni na kuibua vitisho vipya dhidi ya haki za makundi hayo.