

20 May 2025, 1:36 pm
Zaidi ya Watoto 450 wilayani kongwa wanapita changamoto ya ukosefu wa mahitaji muhimu
Na Seleman Kodima.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mayeka Saimon amewataka wazazi na walezi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaambia watoto wao wafeli mitihani ili kuwakatisha masomo huku sababu ikiwa ni kushindwa kuwahudumia mahitaji ya shuleni ikiwamo Sare za Shule.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kukabidhi Msaada wa Sare za Shule na mahitaji mengine ya kujifunzia kwa wanafunzi 105 kutoka Shule saba katika kata ya Kibaigwa wilaya kongwa ambapo Msaada huo umetolewa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA kwa kushirikiana na Shirika la Dutcha water Operator( VEI).
Awali akielezea kuhusu msaada huo Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya maji na Usafi wa mazingira Dodoma Bi Rahel Muhando amesema Mamlaka hiyo wanatambua umuhimu wa kushirikiana na jamii .
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa Mwl Master Mwashala ,sambamba na Mwakilishi wa walimu wakuu wa Shule saba ambazo wanafunzi wake wamepata msaada Loishooki Mollel wameziomba taasisi nyingine kuwatazama watoto hao ili kuwawesha kupata mahitaji muhimu.
Pamoja na hayo inaelezwa kuwa zaidi ya Watoto 450 wilayani kongwa wanapita changamoto ya ukosefu wa mahitaji muhimu hivyo hatua ya Mamlaka ya maji na Usafi wa mazingira Dodoma na VEI kutoa msaada kwa watoto 105 ni Nuru kwa Kundi hilo katika kufanikisha upatikanaji wa Elimu Bila Vikwazo.