Dodoma FM

Chihoni waomba serikali kuwasaidia ukarabati wa madarasa

5 March 2024, 6:48 pm

Picha ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Chihoni Sylvester Chimombo akiongea na Dodoma Tv.

Endapo Ukarabati wa madarasa hayo utafanyika utaweka miundombinu ya shule hiyo katika hali ya usalama kwa wanafunzi katika ujifunzaji.

Na Mindi Joseph.

Wanachi katika Mtaa wa Chihoni kata ya Nala wameiomba serikali kuwasaidia ukarabati wa madarasa 4 ya shule ya Msingi Chihoni.

Uchakavu wa madarasa hayo yakikarabatiwa hakutakuwa tena na uhitaji wa mabarasa kwa shule hiyo yenye zaidi ya wananfunzi 1000.

Tumezungumza na Mwenyekiti wa Mtaa wa Chihoni Sylvester Chimombo na ameyabainisha hayo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Chihoni .

Kwa upande wao wananchi wanasema serikali iwasaidie kukarabati madarasa ili kuboresha miundombinu hiyo.